Majangili wazidi kuritia hasara Taifa. - KULUNZI FIKRA

Monday 26 February 2018

Majangili wazidi kuritia hasara Taifa.

Watuhumiwa 2,617 wa ujangili wamekamatwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 katika maeneo ya mapori ya akiba ,mapori tengefu na hifadhi za jamii (WMA) huku kampuni sita zilizo chini ya Mfuko wa Kusaidia Uhifadhi wa Friedkin(FCF) zikitumia Sh4.5 bilioni katika vita dhidi ya ujangili

Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa ushirikiano pia na maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori(Tawa) ambao kisheria ndio wanasimamia maeneo hayo.

Akizungumza na kulunzifikra blog Leo Jumatatu Februari 26, 2018, Meneja Miradi wa FCF, Nana Gross Woodley amesema watuhumiwa hao wa ujangili walikamatwa katika maeneo sita yenye zaidi ya eka 2.8 milioni ambayo kampuni zilizo chini ya mfuko huo zinafanya kazi za uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na uhifadhi.

Kampuni hizo ni Tanzania Game Tracker Safari, Wenget Windrose Safari na Mwiba Holdings.

Maeneo ambayo kampuni hizo zimewekeza ni Pori la akiba la Maswa; maeneo ya Mbono na Kimali; eneo la Mwiba Ranchi na Hifadhi ya Jamii ya Makao wilayani Meatu; eneo la Uvinza; Pori la Akiba ya Ugala Kusini na Kaskazini; Pori la Akiba ya Moyowosi eneo la Kusini na Pori Tengefu la Ziwa Natroni.

Woodley amesema katika kipindi cha miaka mitatu, kila mwaka FCF imekuwa ikitumia kati ya Sh1.4 bilioni hadi Sh1.7 bilioni katika vita dhidi ya ujangili ikiwemo kununua magari, kuajiri askari ulinzi, kununua vifaa vya ulinzi na kuendesha operesheni mbalimbali dhidi ya ujangili.

Amesema kutokana na jitihada za FCF, kwa kushirikiana na Tawa na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama, matukio ya ujangili yamepungua kutoka 1,226 mwaka 2013 hadi 721 mwaka 2015.

Akitoa mchanganuo wa majangili waliokamatwa katika kipindi cha miaka mitatu, amesema majangili wa nyama kwa ajili ya chakula waliokamatwa ni 304, majangili wa tembo 18, majangili wa mbao 283, majangili wa urinaji asali sita na majangili ya uvuvi haramu 142.

"Katika kipindi hiki cha miaka mitatu 2013 hadi 2015, tumekamata wafugaji waliongiza mifugo hifadhini 853, majangili waliokuwa wakichoma mikaa 82, waliokuwa wameingia hifadhini kinyume cha sheria 881,walioingia kuchoma moto hifadhini 49,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Popular