Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vicent Mashinji amesema kada wa chama hicho, Richard Hiza Tambwe amefariki dunia wakati akiwa mbioni kuteuliwa kuwa mkuu wa propaganda na uenezi wa chama hicho.
Dkt Mashinji ameeleza hayo Jana Februari 10, 2018 wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mwanasiasa huyo iliyofanyika nyumbani kwake Mbagala Kizuiani wilayani Temeke.
Hiza aliyezaliwa mwaka 1959 alifariki ghafla Februari 8, 2018 nyumbani kwake eneo la Mbagala Kizuiani wakati akijaribu kuwahi hospitali kupata matibabu ya pumu.
Hiza aliwahi pia kuwa mwanachama cha NCCR-Mageuzi, CUF na CCM, mara ya mwisho alionekana jukwaani Februari 7, 2018 eneo la Tandale kwa Tumbo akiwa miongoni mwa wanachama wa Chadema waliokuwa wakimnadi mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu.
Akitoa salamu za shukrani, Dkt Mashinji amewaeleza waombelezaji hao kuwa wiki tatu zilizopita aliwasiliana na Hiza ili kujua namna ambavyo ataweza kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.
Amesema Hiza alimpelekea mpango mkakati wa namna atakavyotekeleza majukumu hayo na akamuahidi kuwa uchaguzi wa marudio wa kumpata mbunge wa Kinondoni ukiisha atakwenda ofisini kwa ajili kuanza kazi hiyo.
“Nilikuwa na matarajio ya kwamba Hiza akimaliza uchaguzi atarudi ofisini ili aanze kunisaidia katika kitengo cha propaganda. Nadhani Mungu ameniambia nisubiri ili nitamfute mwingine kwa sababu Hiza amempenda zaidi,” amesema Dkt Mashinji.
Msiba huo uliohudhuriwa na mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam ambao walipata fursa ya kutoa heshima zao mwisho. Hiza amezikwa leo katika makaburi ya Chang’ombe.

No comments:
Post a Comment