Jeshi la polisi linawashikilia vigogo wawili kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. - KULUNZI FIKRA

Wednesday 21 February 2018

Jeshi la polisi linawashikilia vigogo wawili kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

 
Jeshi la Polisi Mwanza kushirikiana na TAKUKURU wamemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Anthony Bahebe na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Alphonce Sebukoto kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Aidha, Kamanda Msangi amesema Bw. Sebukoto alikamatwa mnamo Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Kwa upande wake, Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale amesema Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bahebe.

"Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa ana kaimu nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo", amesema Mhandisi Ernest.

Mnamo Februari 19, 2019 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi alimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.

No comments:

Post a Comment

Popular