Ajali ya basi yaua na kusababisha majeruhi. - KULUNZI FIKRA

Friday 23 February 2018

Ajali ya basi yaua na kusababisha majeruhi.

 
BASI la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake kati ya Kaisho, Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha kifo cha kondakta wa basi hilo.

Kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali teule ya Nyakahanga na wengine katika Kituo cha Afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali.

No comments:

Post a Comment

Popular