Wakazi wa Kijiji cha Mwakitolyo, katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamelazimika kuzuia msafara wa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso kwa kupanga madumu ya maji barabarani,
Wananchi hao walifikia uamuzi huo kwa kishinikiza serikali kuwapatia majibu ya lini watatatuliwa kero ya uhaba wa maji ili waepukane na mateso ya kunywa maji ambayo siyo salama pamoja na kutesa .
Mara baada ya kuzuiliwa na wananchi hao, na kushuka kuwasilikiza kilio chao cha kulazimika kutembea umbali mrefu kuyatafuta maji pamoja na kuuziwa kwa gharama kubwa kwa ndoo yenye ujazo wa lita 20, naibu waziri huyo aliwataka wakandarasi waliopewa jukumu la kujenga mradi maji katika mkoa huo kuongeza jitihada ili kuwasaidia wananchi hao.
Naibu waziri huyo pia akawataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kutoa majibu ya ni lini wananchi wa Mwakitolyo wataondokana na adha ya ukosefu wa maji ambapo katika majibu na ahadi zao walimuahidi naibu waziri huyo kuwa mradi huo unataraji kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji iliyoanza mwaka 2014 hasi sasa ambayo haijamilika katika vijiji vya Mendo, Mwakitolyo na Solwa, Naibu Waziri wa Maji huyo amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano haitowafumbia macho wakandarasi wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitekeleza miradi yao chini ya kiwango

No comments:
Post a Comment