Wabunge nchini Gabon wamebadilisha Katiba ya nchi hiyo, na kuondoa ukomo wa mihula kwa Rais, kinyume na ilivyokuwa awali ambapo alihudumu kwa mihula miwili, kila muhula miaka saba.
Hii inamaanisha kuwa Rais wa sasa Ali Bongo anaweza kusalia madarakani kwa muda mrefu iwapo atachaguliwa na raia wa nchi hiyo.
Rais ataendelea kuhudumu muda wa miaka saba, lakini pia hawezi kufunguliwa mashtaka hata baada ya kuondoka madarakani.
Upinzani umepinga mabadiliko hayo, ambayo wamesema yanalenga kumsaidia Rais Bongo kuendelea kuwa madarakani.
Tabia hii ya kubadili katiba imekuwa ni kawaida kwa viongozi wa nchi za Afrika wenye uchu wa madaraka.
Hii imeshuhudiwa nchini Uganda, Burundi, na nchi nyingine barani Afrika.
Wadadisi wanasema viongozi makatili ndio wanaonekana kufanya hivyo ili kuendelea kusalia madarakani hadi kufa kwao au wanapopinduliwa kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Tunisia Zine El Abadine Ben Alli, Marehemu Mobutu Sese Seko na wengineo.

No comments:
Post a Comment