Uzalishaji wa dhahabu kwa kampuni ya Acacia wazidi kushuka. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 24 January 2018

Uzalishaji wa dhahabu kwa kampuni ya Acacia wazidi kushuka.

 
Kampuni ya uzalishaji dhahabu ya Acacia Mining imetoa ripoti ya uzalishaji dhahabu kwa robo ya mwisho ya mwaka 2017 (kuanzia tarehe 1 Septemba hadi 31 Disemba) mwaka ikionyesha uzalishaji dhahabu umeshuka kwa asilimia 30% ikilinganishwa na robo ya mwisho ya mwaka 2016

Kampuni hiyo imeonyesha uzalishaji wa dhahabu ulifikia kilo 4209.252145 kutokakana na mgodi wa Bulyanhulu kupunguza uzalishaji

Tarehe 4 Septemba kampuni hiyo ilitangaza uamuzi wa kupunguza uzalishaji kwenye mgodi wa Bulyanhulu kutokana na matatizo ya kifedha yaliyosababishwa na serikali ya Tanzania kupiga marufuku makinikia kutolewa nje ya nchi mwezi Machi 2017

Kiasi cha dhahabu kilichouzwa kwa mwaka mzima kilifikia kilo 16807.32663, hiyo ikiwa ni sawa na kushuka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na mwaka 2016 kutokana na makinikia kuzuiwa.

Bulyanhulu ni moja ya migodi mitatu Acacia inayoiendesha , nyingine ikiwa ni Buzwagi na North Mara. Mapato kutoka migodi hiyo mitatu yanafikia asilimia 30 ya jumla ya mapato ya kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular