Shaka azidi kuwatunishia misuli Bavicha. - KULUNZI FIKRA

Friday, 12 January 2018

Shaka azidi kuwatunishia misuli Bavicha.

"Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) ni vyema wakachunga ndimi zao kwani siasa za maji taka zimepitwa na wakati kwa vile vijana hao hawana upeo wa kisiasa, wavivu wa kubuni, kutafakari na kufikiri"

Tunapoizungumzia Serikali CCM ndio wenye dhamana ya kuisimamia Serikali, UVCCM tulishiriki kamilifu kuhakikisha tunatafuta kura za kutosha za Chama Cha Mapinduzi kushika dola na tukafanikiwa hivyo leo kwa gharama yoyote tutamlinda Mhe Rais Dk. Magufuli kwa yeyote atakayejaribu kumdhihaki, kumkebehi, au kutaka kumuondolea heshima.

"Wakiendelea na upuuzi wao BAVICHA tutashuhulika nao UVCCM tumeamua kulinda hadhi na heshima ya Rais wetu ambae ndie Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Joseph Magufuli."

"Nawashauri BAVICHA wafanye tafakuri ya kutosha kama vijana wamshauri Mwenyekiti wao Mbowe na chama chao namna ya kukinusuru na kifo kwani Chama kimeshawashinda na sasa kinachungulia kaburi."

" Huu ni ubashiri kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais Magufuli tunakwenda 2019 chaguzi za Serikali za mitaa na vijiji na uchaguzi wa dola 2020 Tanzania hatuna upinzani ila tutakuwa na mfano wa upinzani kwa vile kazi ya kufanya siasa ya kupambana na CCM wenzetu imewashinda njiani sasa wameishia kufanya siasa ya maji taka"

"Kundi la BAVICHA ikiwa wanataka kufanya siasa nawashauri kutenga muda wa kuipekuwa historia na kuifahamu kabla ya kukurupuka, kuogopa, kuzua au kuongozwa na pupa ya mambo "

"Kuhusu madai ya Lissu mara kadhaa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limetoa taarifa za kulipia gharama za matibabu ya Lissu katika hospitali ya Nairobi na watanzania wote tumeshuhudia vielelezo hivyo."

"Malipo ya ya fedha za umma yana taratibu zake na si kila anayeumwa atalipiwa kwa kadri anavyohitaji kwani fedha za umma zina nidhamu ya matumizi tofauti na fedha za ruzuku zinapofika mikononi mwa CHADEMA."

"Lissu ni muongo kwani Tanzania haina historia ya kuua wanasiasa wanaokosoa Serikali toka awamu ya kwanza hadi ya tano hivyo haiwezi kupanga njama ya kumshambulia lissu kama anavyodai"

"Upo ushahidi unaoonyesha baadhi ya wanasiasa waliokamatwa na kuthibitika kutaka kuindosha kwa mtutu wa bunduki Serikali iliokuwa madarakani walisamehewa na hawakupigwa risasi"

"Namshauri na kumtaka Lissu kama anavyojitahidi kusoma sheria asome na historia ili asiwe kihio na maamuma wa mambo ya nchi yake"

"Wapo waliotaka kuipindua Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere ili kuleta ghasia na machafuko walipukamatwa nakuhojiwa, walipuuzwa na wengine kuachiwa huru"

"Baadhi ya waliowahi kukabiliwa na mshitaka ya uhaini ni Oscar Kambona, Selemani Lipangile, Juma Thomas Zangira, Michael Kamaliza, Agrey Mataka, William Makori Chacha, John Dunstun Liffa Chi-paka, Otin Kambona, Alfred Milinga na Libalo"

" Tanzania kabla na baada ya uhuru imekuwa mstari wa mbele kupigania haki za binadamu, kupinga ubaguzi wa rangi, kutofungamana na siasa za upande wowote na kushiriki harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika"

"Baadhi ya wabunge kusimamishwa bungeni nii kukithiri utovu wa nidhamu na vitendo vyao kwenda kinyume na taratibu za kibunge ikiwemo kutaka kuligeuza bunge tukufu kama kijiwe cha wahuni"

"Wanasiasa kuacha vyama vyao kwenda Ikulu kuisifu utendaji wa Serikali au kurudi CCM ni kuvutiwa na utendaji wa serikali jinsi zinavyowatumikia wananchi kwani hata baada ya uhuru viongozi na wafuasi wa ANC, AMNUT na UTP waliviacha vyama vyao na kujiunga TANU"

No comments:

Post a Comment

Popular