Rais John Magufuli amerudia kauli yake ya kupiga marufuku ya michango kwa shule za msingi na sekondari za serikali na kuagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya viongozi na watendaji ambao maeneo yao yaliwatoza wanafunzi michango mbalimbali kinyume na muongozo uliotolewa na Serikali wa utoaji wa elimu bila malipo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Ikulu Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo.
Rais Magufuli amesema Serikali inatoa takribani shilingi bilioni 23.875 kila mwezi kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa elimu bila malipo lakini anashangaza kuona bado kuna walimu wanaendelea kuwatoza michango ama kuwarudisha nyumbani wanafunzi ambao wanashindwa kutoa michango hiyo.
“Nawaagiza mawaziri, sitaki kusikia mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kutoa michango, na fikisheni maagizo haya kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wote wanaohusika, nikisikia tena mahali jambo hili linaendelea hawa niliowateua mimi wataondoka.
“Haiwezekani tumefuta ada, halafu walimu wanaamua kuanzisha michango tena mikubwa ambayo watu masikini wanashindwa kusomesha watoto wao, na kama wazazi wanataka kuchangia kitu shuleni wapeleke michango yao kwa Mkurugenzi, lakini sitaki kusikia mwanafunzi anapewa sharti la kutoa mchango ndipo apokelewe shule” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya kupata taarifa kuwa zipo baadhi ya shule ambazo wanafunzi wanadaiwa michango mbalimbali tena kwa kiwango kikubwa ikiwemo chakula, maabara, madawati na ziara za kujifunza, hali iliyosababisha wazazi kushindwa kumudu.
Waziri Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ameagiza walimu na viongozi wa halmashauri kuwarudisha shule mara moja wanafunzi wote waliorudishwa nyumbani kwa kutotoa michango na pia kurejesha mara moja michango iliyokusanywa kinyume na mwongozo wa Serikali.
Kwa upande wake, Waziri Jafo amewaagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuwasilisha taarifa ya shule ambazo zimetoza michango kinyume na mwongozo wa Serikali ifikapo Ijumaa wiki hii ili hatua zichuliwe dhidi ya walimu na maafisa elimu ambao kwa makusudi wamekiuka mwongozo huo.

No comments:
Post a Comment