RAIS John Magufuli amesema anatambua mchango mkubwa wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru katika siasa na maendeleo ya nchi.
Alisema hayo jana alipokwenda kuwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam, akiwemo Kingunge na mapacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu jana ilisema katika wodi ya Mwaisela, Rais Magufuli alimjulia hali Kingunge ambaye anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa wake, nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilisema Dk Ibrahim Mkoma wa hospitali hiyo alimueleza Rais Magufuli kuwa hali ya Kingunge inaendelea vizuri. Katika hatua nyingine, Kingunge alimshukuru Rais kwakwenda kumuona hospitalini hapo na amemueleza kuwa sasa anajisikia nafuu baada ya kupata matibabu.
Pamoja na kumpa pole na kumuombea apone haraka, Rais Magufuli alisema anatambua mchango mkubwa wa Kingunge katika siasa na maendeleo ya nchi. Katika wodi ya Sewahaji, Rais Magufuli alimjulia Richard Kajumulo ambaye ni Kaka wa Mbunge wa Muleba Kusini Profesa.
Anna Tibaijuka, Said Abeid Salim, Amina Shirwa, Mzee Hamad Lila na amempa pole Naibu Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk Zainab Chaula aliyefiwa na mama yake mzazi wakati Rais akiwa wodini humo.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amewajulia hali mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti, ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa matibabu ya moyo. Maria na Consolata walimshukuru Rais Magufuli kwa kwenda kuwaona na kuwapa pole na pia wameongoza sala ya kumuombea Rais na nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi alisema matibabu kwa Maria na Consolata ambao ni wanafunzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Ruaha (RUCU) yanakwenda vizuri.
Aidha, Profesa Janabi alisema taasisi hiyo imefanikiwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa moyo 1,400 katika mwaka uliopita na kwamba inashika nafasi ya tatu Barani Afrika kwa utoaji wa huduma bora za matibabu ya moyo.
Rais Magufuli aliwashukuru na kuwapongeza madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kwa kazi kubwa wanayofanya kutibu wagonjwa na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili ili kuboresha huduma zaidi.
“Nawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote, mnafanya kazi kubwa ya kuwatibu wagonjwa, pia mmeboresha hospitali na inaonekana ni safi, mimi niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira yenu ya kazi ili muendelee kutoa huduma nzuri,” alisema Rais Magufuli

No comments:
Post a Comment