Nzi watumika kugundua nyama salam. - KULUNZI FIKRA

Monday, 15 January 2018

Nzi watumika kugundua nyama salam.

Wauzaji nyama nchini Uganda pamoja na wateja wao sasa wanategemea nzi kama kielelezo cha kuangalia ubora wa nyama inayouzwa kwenye maduka husika.

Hii inafuatia operesheni inayoendeshwa na halmashauri ya mji ambapo wauza nyama walaghai hutumia kemikali na dawa hatari kwa afya ya binadamu kuhifadhia nyama.

Matokeo ya haya tangu mwanzoni wa mwaka huu ni mienendo ya wateja kusita kununua nyama na samaki, hali ambayo imeathiri pakubwa biashara ya bidhaa hizo.

No comments:

Post a Comment

Popular