Waziri wa mambo ya ndani Dkt Mwigulu Nchemba, ametangaza kusimamisha zoezi la hati za kusafiria za jumla na kwa makundi mpaka pale utakapowekwa utaratibu wa kuendelea kufanya hivyo.
Waziri huyo alitoa tamko hilo aliafanya ziara katika Ofisi za Uhamiaji na kusema hii ni kutokana na kuwepo taarifa za vijana wanaoenda nje kukumbwa na unyanyasaji, kufanyishwa kazi katika madanguro, kutumiwa katika usafirishaji wa madawa ya kulevya,
Dkt Nchemba amesema Serikali itaandaa utaratibu mzuri kati ya Tanzania na nchi husika wanakokwenda wahusika ili waandaliwe mazingira mazuri na salama ya kufanyia kazi na kujiridhisha na kile wanachokwenda kufanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 25,2018 Dkt Nchemba amesema baadhi ya matendo yanayokiuka sheria za nchi wanayofanyiwa ni kazi zisizo na maadili na kuwekwa rehani kutokana na masuala ya dawa za kulevya.
Dkt Nchemba pia ameagiza kampuni zinazoingiza makundi ya watu wanaokuja kufanya kazi nchini kuripoti leo kwa kamishna wa mipaka na vibali.
Agizo hilo amesema linatokana na baadhi ya kampuni hizo kuwatafutia kazi raia wa kigeni na wanapofika nchini hufanya kazi tofauti ikiwemo biashara ya ngono.

No comments:
Post a Comment