Mtatiro afunguka kuhusu marudio ya uchaguzi mdogo nchini. - KULUNZI FIKRA

Monday, 22 January 2018

Mtatiro afunguka kuhusu marudio ya uchaguzi mdogo nchini.

 
"Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetenga bajeti ya Shilingi Bilioni 1 (Milioni 1000) FEDHA ZA WALIPA KODI MASIKINI, ili kusimamia uchaguzi wa jimbo la Kinondoni - Dar es salaam", alisema Mtatiro.

"Serikali yetu inazo Shilingi Bilioni 1 za kusimamia uchaguzi ambao umelazimishwa na serikali hiyo hiyo ambayo imemfanya aliyekuwa mbunge kuwa bidhaa na kisha inamrejesha sokoni ili anunuliwe tena", alisema Mtatiro.

"1 Billion ni sawa na Pikipiki 500 mpya ambazo zingeteneza ajira mpya 500 kwa vijana 500 na kuzaa faida ya shilingi Bilioni 1.44 kwa mwaka mmoja", alisema Mtatiro.

"Shs Bilioni 1 zinaweza kununua matrekta madogo ya kilimo yapatayo 100 ambayo yanaweza kulima ekari 30,000 kwa mwaka na kuzalisha mazao yenye thamani ya mabilioni ya pesa", alisema Mtatiro.

"Shs Bilioni 1 zinaweza kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa vijana 220 kwa mwaka mzima, na vijana hao 200 wakaja kuzalisha mabilioni ya pesa kwenye uchumi wa nchi", alisema Mtatiro.

"Shs Bilioni 1 zinaweza kulipa mshahara wa mlinzi kwa mwaka mzima kwenye jumla ya shule 555 nchi nzima na kwa hiyo migogoro ya shule kuchangisha wazazi pesa za walinzi ikafia hapo", alisema Mtatiro.

"Shilingi Bilioni 1 zinaweza kuanzisha jumla ya biashara 2,000 kwa wajasiriamali 2000 wadogo ambao kila mmoja anaweza kuzalisha faida ya Shilingi 200,000 - 300,000 kwa mwezi na kwa ujumla wakazalisha Shilingi Bilioni 4.5 kwa mwaka mmoja, kama faida", alisema Mtatiro.

"Lakini, kinchi masikini na ombaomba kama hiki cha kwetu, kimejiingiza kwenye biashara ya kununua wabunge na madiwani, na matokeo yake badala tutumie fedha za serikali kuzalisha ajira, kupanua mitaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu wetu - tunatumia fedha hizo ili kufanyisha uchaguzi mpya ambao utapelekea wabunge wabadilishe vyama na kuingia CCM?",alihoji Mtatiro.

"Mambo mengine yanahitaji akili ndogo kweli! Mngeliweza kusubiri 2020 mkanunua wabunge na madiwani wote wa upinzani. Na kati ya 2015 - 2020 mkatumia kila SENTI yenu kuzalisha ajira na kukuza uchumi. Badala yake, muda huu wa kuzalisha ajira na kukuza uchumi ndipo mnatumia fedha za walipa kodi kununua madiwani na wabunge na kurudua chaguzi", alisema Mtatiro.

"Ikifika 2020 mtakuwa mmeumiza maisha ya familia ngapi? Mtakuwa mmewanyima vijana wangapi mitaji? Mtakuwa mmewapora vijana wangapi bodaboda? Mtakuwa mmewaua wakulima wangapi wanaolima kimasikini kwa jembe la mkono?", alihoji Mtatiro.

No comments:

Post a Comment

Popular