Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amefunguka na kuweka wazi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Mhe Edward Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais John Pombe Magufuli toka siku nyingi.
Gambo amesema hayo Jana Januari 10, 2018 akiwa anaongea na waandishi wa habari na kudai kuwa amefurahishwa kuona kiu hiyo ya Lowassa kukutana na Rais Magufuli imefikiwa jana pale Ikulu na kudai kuwa hata wao kama viongozi wameweza kujifunza jambo kutoka kwa Rais Magufuli kukubali majadiliano na kiongozi huyo wa upinzani.
"Ni kweli kwamba Mhe. Lowassa alikuwa na kiu kubwa ya kukutana na Rais na Mtanzania yoyote mwenye akili timamu lazima awe na kiu hiyo ya kumuona Mhe. Rais kwa sababu yeye ndiye Rais wetu Watanzania, yeye ndiye amepewa dhamana kutuletea maendeleo sisi kama taifa kwa hiyo mtu yoyote hata kama si Mtanzania ana jambo lake lolote la kimaendeleo njia nyepesi ya kulifanikisha ni lazima ampitie mtu ambaye amepewa mamlaka na Watanzania." alisema Mrisho Gambo
Aidha Gambo alitumia nafasi hiyo naye kumpongeza Rais John Pombe Magufuli
"Nampongeza Mhe Rais kwanza kwa kuonesha ajenda yake kubwa ni maendeleo kwamba uchaguzi alishamaliza 2015 sasa hivi anajielekeza kwenye maendeleo, ni Rais ambaye hana ubaguzi ameshakutana na viongozi wengi wa dini, wanasiasa na amekutana na makundi mbalimbali. Rais jana ametufundisha uongozi hasa zaidi sisi viongozi vijana" alisisitiza Mrisho Gambo.
Januari 9, 2018 kiongozi wa CHADEMA ambaye aligombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa alimtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaama na kumpongeza kwa kazi nzuri anazofanya.

No comments:
Post a Comment