Meya wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mhe Alex Kimbe amedai alipigiwa simu na watu wawili ambao amewataja kuwa ni Michael Mlowe kutoka CCM na diwani wa Kihesa viti maalum, ambao walimuita na kwa kuwa anafahamiana nao akaenda akidhani wana jambo la msingi la kumuambia.
Lakini moja ya vitu walivyovizungumza ni kumuambia aachie nafasi ya umeya na kumuahidi kiasi cha fedha yeye alikataa na kusema heshima aliyopewa ni kubwa kuliko fedha wanazotaka kumpa.
Amesema bado aliendelea kupigiwa simu na namba ambazo hazifahamu na kuendelea kumsisitiza ahamie CCM.
Ameendelea kueleza baada ya kumuona hataki kuhama walianza kumtishia kumfunga kwenye kesi yake ya kumtishia mtu kwa bastola.
Meya huyo amesema madiwani wa CHADEMA wa Iringa Mjini wamefikia 8 na wengine wakiwa ni wa viti maalumu na kuwaomba radhi wananchi wa Iringa kutokana na hilo
Amesema walianza kununuliwa kwa dau la milioni 8 hadi 10, lakini waliohamia mwishoni wamenunuliwa kwa milioni 20 hadi milioni 30.
Meya huyo ameeleza ili kuthibitisha wamepewa rushwa, madiwani hao baada ya kuhama CHADEMA wamenunua magari na kujenga nyumba

No comments:
Post a Comment