Mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe Freeman Mbowe amedai amesikitishwa na namna inavyoendeshwa kesi ya Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga iliyoahirishwa Jana.
Mhe Freeman Mbowe ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii Jana katika viunga vya Mahakama ya mkoani Mbeya mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na kuzitaka mamlaka husika zinazosimamia sheria nchini kujiangalia vizuri katika utendaji kazi wake.
"Tumesikitishwa kwa namba suala hili jinsi lilivyo shughulikiwa, sipendi kuingilia uhuru wa Mahakama, mienendo ya kimahakama lakini mimi kama raia na kiongozi nafikili vyombo vinavyostahili kutoa haki kwa wananchi vinawajibu wa kujiangalia vizuri. Mahakimu, Majaji, Mawakili wa Serikali pamoja na Askari wenyewe hawa wote ni binadamu haina maana kwamba wao hawawezi kufanya makosa wao ni binadamu kama walivyo wengine", alisema Mhe Mbowe.
Kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga imehairishwa leo na kutajwa kusikilizwa Februari mbili baada ya Mawakili watatu kujitoa kuwasimamia katika kesi hiyo.

No comments:
Post a Comment