Kaya 362 zakosa makazi. - KULUNZI FIKRA

Sunday, 21 January 2018

Kaya 362 zakosa makazi.

Kaya  zaidi ya 362 mkoani mtwara zakosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na shule tatu za msingi kuezuliwa paa katika vijiji vya Mkwedu wilaya ya Tandahimba baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha mkoani humo.

Katika tukio hilo watu wanne wa familia moja walijeruhiwa huku vyombo vyakula na mifugo vikiharibiwa.

Baadhi ya viongozi wa seerikali wameanza kutoa misaada ya kibinaadamu ili kuzinusuru kaya hizo. “Mimi pamoja na kamati yangu ya siasa ya mkoa tumejitokeza  na kuchangia mifuko mia moja na hamsini ya unga na mifuko sabini ya maharage. Ninawasihi wakazi wengine ambao wako katika hali nzuri, kujitokeza na kuwasaidia wahanga hawa,” Yusuph Nnanila Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara alisema.

No comments:

Post a Comment

Popular