Idara ya usalama ya Cameroon kwa kushrikiana na vikosi vya nchini Equatorial Guinea wamefanikiwa kuyazima mapinduzi yanayodaiwa kuratibiwa na watu wasioitakia mema nchi hiyo, kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo.
Takriban wanaume 30 waliojihami kutoka Chad, Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya kati walikamatwa mwezi uliopita, alisema waziri mmoja.
Walikamatwa wakiwa mpango wa kuzindua silaha za milipuko, bunduki na risasi kwenye mpaka wake na nchi ya Cameroon.
Serikali ya Rais Teodoro Obiang Nguema, imekuwa ikituhumiwa kukithiri kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.
Wanajeshi nchini Equatorial Guinea wamewaua kwa kumpiga risasi watu hao waliokuwa kwenye mpango huo wakati wa mapigano jana karibu na mpaka na Cameroon, kwa mujibu wa runinga ya taifa TVGE.
Obiang amekuwa madarakani kwa takribani miaka 40, baada ya kutwaa kuongoza mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979 na kumuondoa madarakani mjomba wake Francisco Macias Nguema ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.
Katika taarfa iliyosomwa kupitia redio ya taifa, Waziri wa Ulinzi, Nicholas Obama Nchama aliwalaumu maadui wa nchi hiyo aliodaiwa kupewa kazi na makundi ya upinzani na kusaidiwa na mataifa ambayo hayakutajwa.

No comments:
Post a Comment