Gari moja lililokuwa linaendeshwa kwa kasi katika jimbo la Califonia hapo jana liliruka na kuingia ndani ya ghorofa ya juu kwenye jumba moja baada ya kugonga uzio wa kutenganisha barabara.
Sehemu moja ya gari ilibaki ikining'inia nje ya jengo hilo huku watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo wakinusurika na majeraha madogo.
Polisi wameambia wanahabari kwamba dereva wa gari hilo anadaiwa kutumia dawa na alikuwa ametembelea hospitali moja.
Ajali hiyo pia ilisababisha kuzuka kwa moto mdogo ambayo wazimamoto walifanikiwa kuuzima.
Kisa hicho kilitokea Santa Ana, maili 35 (56km) kusini mwa Los Angeles.

No comments:
Post a Comment