Chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC, kimethibitisha kuwa kinajadili utaratibu wa kuondoka madarakani kwa Rais Jacob Zuma.
Hata hivyo, haijakubaliwa tarehe rasmi ya kuachia madaraka kwa Rais Zuma, kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Duru kutoka ndani ya chama hicho, zimesema kuwa Rais Zuma ambaye anatuhumiwa kuhusika na matukio mbalimbali ya ufisadi ameshauriwa kujiuzulu mwenyewe la sivyo ataondolewa kwa nguvu na chama hicho.
Shinikizo zimekua zikiongezeka kwa Rais Jacob Zuma kutakiwa kujiuzulu nafasi yake kabla ya uchaguzi mkuu wa hapo mwakani. Hivi karibuni Bunge nchini humo lilitangaza kuwa linatazamia kujadili hatua za kuchukua kumuondoa rais Zuma Madarakani.
Uamuzi huu wa bunge ulikuja ikiwa ni siku chache tu zimepita toka mahakama ya katiba nchini humo kuamua kuwa bunge lilishindwa kumuwajibisha rais Zuma kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kufanya ukarabati kwenye makazi yake binafsi.

No comments:
Post a Comment