JINAMIZI la kuhamwa na wawakilishi wa wananchi, viongozi na wanachama wa vyama vya CHADEMA na CUF limeendelea kuvikalia kooni vyama hivyo. Ambapo mara hii madi
wani wawili wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, mkoa wa Lindi wamehamia Chama Cha Mapinduzi.
Madiwani hao, Bakari Mpanyangula (CUF) wa kata ya Nachingwea, na Ibadi Mbute (CHADEMA) kata ya Namichiga ambao walitoa matamko yao juzi kwa nyakati tofauti kwenye kata zao, walieleza sababu zilezile ambazo zimekuwa zikitolewa na wawakilishi, viongozi na wanachama wanaohama kutoka katika vyama hivyo kwenda CCM.
Walisema wamehamia CCM ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Madiwani hao wamesema pamoja na kupambana na ufisadi, uzembe, rushwa na ukwepaji wa kulipa kodi lakini imejitahidi kuboresha masilahi ya wakulima. Hususani wakulima wa zao la korosho.
"Licha ya juhudi za Mhe Rais Magufuli na timu yake yote, lakini namuunga mkono mbunge wa jimbo letu la Ruangwa, mhe Kassim Majaliwa kwanamna anavyojitajidi kusukuma maendeleo katika jimbo letu. Sasa nimeona niungane nae kwa nia njema kabisa ya kusukuma maendeleo nikiwanae kwenye chombo kimoja, alisema Mpanyangula, diwani wa kata ya Nachingwea.
Mpanyangula aligusia mgogoro wa uongozi unaoendelea kurindima ndani ya chama cha CUF. Nakufichua kwamba mgogoro huo umesababisha kikose mwelekeo. Hivyo kwa watu wenye dhamira ya kweli ya kupenda maendeleo wataendelea kukikimbia.
Nae diwani wa kata ya Namichiga, Ibadi Mbute alisema uamuzi aliochukua ni sahihi na amefanya kwa ajili ya masilahi mapana ya jimbo la Ruangwa na taifa kwa jumla. Akibainisha kwamba juhudi za serikali ya awamu ya tano hazina budi kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo. Tena akiwa ndani ya chama kilichounda serikali hiyo(CCM)
Kujiuzulu kwa madiwani hao kumepunguza idadi ndogo ya madiwani wa vyama vya upinzani, miongoni mwa 30 wanaounda baraza la madiwani la halmashauri hiyo.Ambapo kabla ya madiwani hao wawili kuhama, CUF kilikuwa na madiwani 7,na CHADEMA diwani mmoja. Wakati CCM kinachoongoza halmashauri hiyo kikiwa na madiwani 22.
Hii ni mara ya kwanza kwa madiwani wa upinzani kuhama vyama vyao najiunga na Chama Cha Mapinduzi. Wakati CCM haijawahi kuhamwa na diwani wala mbunge nakujiunga na vyama vya upinzani vilivyopo wilayani humo.

No comments:
Post a Comment