TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza utaratibu wa familia za kabila la Kichaga kutumia majani maarufu kama ‘sale’ kufunika au kumaliza kienyeji kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia na mimba za wanafunzi.]
Majani hayo ya masale kwa mila na tamaduni za kabila la Wachaga, hutumika kuashiria amani, kuomba msamaha na kumaliza tofauti zao.
Ofisa wa Takukuru Wilaya ya Hai, Denis Mazigo, alifichua siri hiyo ya kuanza kwa uchunguzi dhidi ya mila hiyo wakati wa uwasilishaji ripoti ya kamati ya ulinzi wa mtoto.
“Haliwezi kutangulizwa jani la sale peke yake, lazima kuna mazingira ya kutolewa kwa fedha kama rushwa, ndiyo msamaha uweze kukubalika. Sasa sisi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeanza kufanyia kazi jambo hili, kwa sababu tumeona kesi nyingi za ukatili zikikwama huku zikiwa na ushahidi wa kutosha,” alisema Mazigo.

No comments:
Post a Comment