MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Pombe Magufuli, amemuomba katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana, kuendelea kuhudumu katika nafasi hiyo.
Taarifa kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam na makao makuu ya chama hicho, Lumumba zinasema, hatua ya Magufuli kumuomba Kinana kuendelea na wadhifa wake inatokana na “kushindwa” kumpata mtu mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo.
Kinana ameripotiwa mara kadhaaa na vyombo vya vya habari kutishia kujiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa hashirikishwi katika uendeshaji wa chama hicho.
Mtoa taarifa wa kulunzifikra blog ameeleza kuwa mkutano wa kumshawishi mwanasiasa huyo ulifanyika wiki mbili zilizopita, Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Kwenye mkutano huo wa Ikulu, ndipo Rais Magufuli alimuomba Komredi Kinana aendelee kukiongoza chama hicho kwa nafasi ya katibu mkuu,” ameeleza mtoa taarifa.
Anasema, kabla ha mkutano huo, Kinana alishaweka wazi msimamo wake wa kung’atuka kwenye uongozi wa juu wa chama hicho tawala.

No comments:
Post a Comment