Kulunzifikra blog imebaini kuwa kwa sehemu kubwa, wazazi waliotengana watoto wakibaki kuishi na mzazi mmoja, ama mama au baba, janga hilo huijitokeza.
Ni hatua na mazingira ambayo watoto wanakosa malezi na matunzo ya wazazi wawili na ndipo udhalilishaji wa kijinsia huchukua nafasi.
Sambamba na nafasi hiyo ya uhusiano wa kifamilia, pia kuna suala la umasikini katika ngazi ya familia, watoto wa kike wanajikuta wanashawishika kupewa zawadi za vitu mbalimbali na hatimaye wanaishia kunasa katika mtego wa ngono na ujauzito kuchukua nafasi yake.
Mrajis wa Elimu Zanzibar, Siajabu SuleimanPandu, anasema utafiti uliofanywa na wizara yake mwaka jana, umegundua kuvunjika kwa ndoa nyingi ni chanzo cha watoto kupoteza mwelekeo na kunasa katika udhalilishaji na hasa kimapenzi.
Anasema ongezeko la kesi za udhalilishaji, ikiwamo mimba za utotoni, watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo wengi ni wasioishi na wazazi wao wawili.
“Kuvunjika kwa ndoa kunasababisha watoto kupoteza mwelekeo na watoto hawana makosa,” anasemaSiajabu na kuongeza: ”Matendo mengi yanayoripotiwa, wafanyaji ni watu wa karibu.”
Anataja sababu nyingine ni utandawazi, dunia hivi sasa ikiwa katika sura ya kiganja, matukio yanayotokea Ulaya yalikuwa hayaonekani Zanzibar, lakini hivi sasa yanaonekana.
Siajabu anafafanua kuwapo utandawazi na mitandao ya kijamii, watoto wanaiga mambo mbalimbali na athari zake zinaishia kwenye vitendo vya udhalilishaji.
Anaeleza sababu nyingine ni wanajamii kushindwa kumaliza tatizo hilo la mimba za utotoni kisheria na wanaishia katika kinachoitwa,“ kumalizana wenyewe kwa wenyewe, katika matukio ya udhalilishaji.”
Kwa mujibu wa Siajabu, hiyo imegeuka kuwa sehemu kuu ya sababu za kuongezeka kwa udhalilidhaji kijinsia.
Ushauri wake ni kwamba, serikali inatakiwa iwezekuongeza ujasiri mkubwa wa kumpabana na wote wanaorudisha nyuma juhudi za kupinga udhalilishaji na kuihindwa kutoa ushahidi wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia.
“Tuondoe muhali na tuone kuwa mahakama zetu zinawatia hatiani watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji ikiwamo mimba za utotoni,”anasema.
Kasoro ya DNA
Anaeleza kilio chake kikubwa kwa kesi za ujauzito na mashine ya uchunguzi wa vinasaba (DNA), pia wadhalilishaji wanaowabebesha ujauzito watoto, wamepata mwanya kutokana na kukosekana DNA za kumtia hatiani mtuhumiwa.
Anasema kama serikali haijatafuta adhabu mbadala ili kuhakikisha kesi hizo zinachukuliwa hatua na wadhalilishaji kuweza kupewa adhabu kali.
“Kama tunahisi hatuna uwezo wa DNA. Serikali ibadilishe sheria ya ushahidi itafute ushahidi mwengine mbadala ambao mtuhumiwa anaweza akachukuliwa hatua za kisheria,”alisema.
Siajabu anasema kuwa, baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kugundua kuwapo kesi 72 za udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa msingi na sekondari kuripotiwa kwa mwaka 2016, ikiwamo ujauzito, ilifanya utafiti kwa shule zote za serikali na binafsi zilizosajiliwa Unguja na Pemba na kugundua uwepo wa kesi 214 za udhalilishaji.
Anaeleza kuwa, kesi 214 ni ambazo hazijaripotiwa wizarani na badala yake familia zilimalizana wenyewe.
Utafiti huo uligundua kwa mwaka huo uwepo wa watoto 74 waliopewa ujauzito na matukio 26 kwa mwaka huo ndio yalitopotiwa, ikiwa ni sawa na asilimia 35 na Siajabu anasema, wizara iliwaruhusu kuendelea na masomo kwa manufaa ya maisha yao ya baadaye.
Anasema waligundua wanafunzi 61 waliozeshwa na 106 wamelawitiwa na kubakwa, wakiwa ni watoto wa kike na kiume.
“Kwa kweli hali ni mbaya. Kama hali hii itaendelea miaka kumi ijayo, sijui tutakuwa na taifa la aina gani,”analalamika Siajabu.
Kutoka kwa Mhusika
Amina Juma, ambaye sio jina lake halisi, aliyepewa ujauzito akiwa na umri wamiaka 16 akiwa kidato cha pili mwaka jana,anasema alipatwa na hilo kutokana na vishawishi baada ya kukosa baadhi ya mahitaji kutoka kwa familia yake.
“Mama na baba yangu walishaachana na nilikuwa nikiishi na mama yangu. Wakati mwingine nahitaji fedha kwa ajili ya matumizi madogo ya shule, nashindwa kuzipata, kwa sababu mama alikuwa hana uwezo na baba alitutelekeza.
“Hivyo,nikashawishika baada ya kupewa fedha kwa ajili ya matumizi na mwanaume mmoja, ambaye alinipa ujauzito,” anasema Siajabu.
Anaongeza kuwa, baada ya kupata ujauzito, aliendelea na masomo na alifaulu mtihani wa taifa wa kidato cha pili na hivi sasa ameshajifungua na anaendelea na masomo kidato cha tatu.
Amina anaongeza kwamba licha ya kujifungua, anaendelea na masomo, ingawaje anakiri kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yake ya sasa.
Anazitaja changamoto hizo kuwa, muda wa kudurusu masomo yake umekuwa ni mdogo kutokana na kuwa na jukumu la kulea mtoto.
“Wakati mwingine nahitaji kubaki na wenzangu shule kwa ajili ya masomo ya ziada, lakini nashindwa kwa sababu mtoto anahitaji kunyonya inanibidi nirudi nyumani nikamlee mtoto wangu,”anasema.
Anaongeza:“Mimi nashukuru wazazi wangu hawajanisusa kutokana na kupata ujauzito, lakini ‘vijineno’ vidogo vidogo havikosekani, hasa pale unapochelewa kurudi nyumbani.”
Anawashauri wanafunzi wenzake kutojiingiza katika masuala ya kimapenzi na badala yake kushughulikia masomo yao.
Anaongeza kuwa:”Kusoma ukiwa na mtoto ni mtihani, inataka moyo na ndio maana baadhi yao wanashindwa maana wakati mwingine unasumbuliwa na wanafunzi wenzako pamoja na jamii, lakini inabidi uvumilie”.
Viongozi wa Shehia
Mratibu wa Wanawake na Watoto katika Shehia ya Melinne, Fatma Juma Jaku,anasema mimba za utotoni bado ni tatizo kubwa katika Shehia yao.
Anasema sehemu kubwa ya mimba hizo haziripotiwi na jamii husika hutumia mbinu ya kumalizana wenyewe, amakwa kuwaozesha watoto waliopewa ujauzito au kulipana fidia.
Kwa mujibu wa Fatma, baadhi ya wanajamii wanaona bora kesi hizo wazimalize wenyewe kwa kusameheana, kutokana na kuvunjika moyo kuhusu mwenendo wa kesi za udhalilishaji mahakamani na katika vituo vya polisi.
Sheha wa eneo hilo,Amani Ayoub Makame,anasema licha ya juhudi anazozichukua katika kutoa elimu ya udhalilishaji, bado matukio yanaendelea.
Anasema elimu zaidi inahitajika kuanzia shuleni hadi katika vyuo vya madrasa, ili watoto wafahamu athari za udhalilishaji.
Lingine analolitaja ni kuwaepuka wafanyaji matukio hayo, ambao baadhi wanadaiwa kutuma njama za kuwapa zawadi watoto.
“Hivi sasa tuwafundishe watoto wetu. Unapoitwa kwenda kuchukua zawadi, ukatae, maana hivi sasa watu wamekuwa waharibifu kwa watoto,”anasema.
Hata hivyo, anawataka wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto, pamoja na jamii kwa ujumla kutovunjika moyo na kuendelea na kasi ya mapambano ya udhalilishaji.

No comments:
Post a Comment