Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Mhe Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.
Komu akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.
“Usahihi ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano, kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,” alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema Mhe Komu.
“Hata hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana… kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania tutakipata?” alihoji Mhe Komu.
Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa... “Watapata jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020 tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.” alisema Mhe Komu.

No comments:
Post a Comment