Mbunge wa Chadema asema upinzani hauwezi kufa kamwe. - KULUNZI FIKRA

Friday, 15 December 2017

Mbunge wa Chadema asema upinzani hauwezi kufa kamwe.

 Nitampiga Mchungaji wa kondoo, na kundi la kondoo watatawanyika. Kisa hiki kinapatikana katika biblia, kitabu cha mathayo mlango wa 31.

 Nini maana ya maneno hayo!! Mchungaji ni kiongozi na kondoo ni wafuasi!! Unapomuondoa kiongozi wa mahala popote wafuasi watakosa muelekeo na kupotea kusikojulikana.

 Wana mkakati wa CCM wanahangaika na kondoo wakati mchungaji bado yupo imara anaongoza wafuasi wake. Huwezi kuua chama cha siasa kwa kununua wafuasi ambao ukiwaambia waitishe ata mkutano wa hadhara hawawezi kufikisha watu 200. Hata watanzania hawawajui mpk siku wanapohama. Hapo ndipo unapotambua kuwa tunatofautiana kiuwezo na kimkakati. Niwaeleze tu vita haipiganishwi kwa idadi kubwa ya wanajeshi wasio na uwezo bali kwa weledi na ubora wa jeshi!!

 Hiki kinachofanyika sasa hata Rais Banda wa Zambia wakati wa MMD alikifanya kununua wabunge upinzani wa PF kilichokua chini ya Mhe Satta. Lakini ilipokuja wakati wa uchaguzi mkuu Marehemu Rais Satta alishinda uchaguzi na kuwa rais wa zambia, akiwa na wapiganaji wachache, mahiri na wenye moyo wa kujitoa( wakati huo alikuwa na 4% tu wabunge). Yanayotokea sasa yanatujenga zaidi kuliko kutukatisha tamaa.

Note: unapohangaika kuua chama kikuu cha upinzani jua kuwa unaua chama chako pia!! Maana endapo utafanikiwa basi kifuatacho kitakuwa ni mass rebellion(uasi wa wananchi dhidi ya utawala wako na chama chako).
    

No comments:

Post a Comment

Popular