Kazi kubwa kabisa ya Mbunge ni kutunga sheria. Zingine ni kazi za ziada tu. Kila mwaka, lije jua ije mvua lazima Bunge litunge sheria inayoitwa “SHERIA YA FEDHA YA MWAKA XXXX/YYYY” hii ni pamoja na sheria zingine “kama itapendeza”
Mbunge anapojiuzuru ubunge kwa kumuunga mkono JPM anakuwa anachanganya madesa. Ana-compromise nafasi ya kuisaidia nchi kwa kutunga sheria makini na kwenda kujificha mgongoni mwa mtu.
Kama Mbunge anaweza kumsaidia JPM kwa kuondoa ama kurekebisha sheria mbovu. Mfano sheria ya:
1. Takwimu
2. Habari
3. Mitandao
4. Fedha 2017/18
......,
Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na sheria pendekezwa ya Vyama Vya Siasa.
Ukiangalia mzigo huu wa kazi, unajiridhisha kuwa hakuna muda wa kupoteza na badala yake ni kukimbizana na wakati ili kukamilisha hili.
Serikali ya awamu ya 5 lazima ijue kwamba yanayotokea sasa ni kujitengenezea anguko lake yenyewe. Turejee sababu za kuanguka kwa himaya ya Roma na Ottoman. Sababu kuu naziona hata hapa kwetu Tanzania zipo, nazo ni:
1. Mdororo wa uchumi (wananchi kukosa fedha huku utawala ukijinasibu kukua kwa uchumi - both Roma & Ottoman).
2. Upendeleo katika uteuzi jeshini. Wanajeshi wanapandishwa vyeo si kwa uwezo wao bali ni kwa ukaribu wao na mtawala (nepotism), hasa wakati wa mfalme Sulleyman wa Ottoman ingawa hata Roma ilikuwepo.
3. Dini kutoridhishwa na uendeshaji wa Serikali: Roma (Ukristo) na Ottoman (Uislamu-the Sufi order)
4. Matumizi ya majeshi ya kukodi (Roma: the Germany mercenaries na Wakurd kwa Ottoman)
5. Bribery: Tunaona jinsi serikali ya TZ inavyotumia rushwa kuhalalisha mambo. Tumesikia malalamiko bungeni ambapo wabunge wa CCM wamepewa 10m kila mmoja ili kupitisha mambo ikiwemo budget kuu. “Yalisemwa hadharani” Madiwani, wabunge na viongozi wa vyama wakinunuliwa ili kuunga mkono Serikali.
6. Luxury/Starehe na anasa. Hili linawezekana kwa hapa kwetu lisiwe wazi kwa sasa lakini wakati wa Mfalme Constantine (Roma) na Sulleyman (Ottoman) hili lilikuwa tatizo kubwa sana. Wafalme hawa walichukuwa wanawake na kustarehe nao, wakaandaa sherehe na hafla ili kujitengenezea utukufu na mpaka wakawa wanachukua wake wa wasaidizi wao kwa tamaa zao na zinaa huku rushwa ikishamiri (ndipo DINI zilijipambanua na kuanza kupinga utawala na watawala).
7. Kufunga jela na kuua wakosoaji wa utawala. Kwa upande wa Roma, imani ilikua sana na Ukristo kushamiri, vivyo hivyo na uislamu kwa Ottoman empires. Dini zilikosoa sana dola na hata viongozi wake kuteswa na wengine kuuawa. Roma walikuwa wanawatupa wapinzani wao kwenye shimo lenye simba wenye njaa. Ottoman waliwaua hadharani wapinzani ili kujenga hofu kwa umma.
8. Kuogopwa kwa mtawala Constantine (Roma) na Sulleyman (Ottoman). Wasaidizi wa watawala hawa wawili hawakuweza kushauri kwa uhuru na ufasaha wakiogopa kutumbuliwa. Kutumbuliwa kwa nyakati hizo kulikuwa kubaya sana ikiwemo kutupwa kwenye shimo la simba wenye njaa.
9. Kununua kura. Chaguzi zilitawaliwa na wagombea kulipa vipande vya fedha kwa wapiga kura. Baada ya matokeo, washindi wa chaguzi hizi walitumia rushwa na ufisadi ili kurejesha ghalama walizotumia wakati wa uchaguzi. Kwa sasa haya tunayaona hapa TZ, CCM hawana muda hata wa kampeni, kazi yao ni kugawa fedha kwa wapigakura na kuvuruga chaguzi.
Nimeona ni vyema tujikumbushe haya ili kumsaidia mtu yeyote anayetupeleka matatani aweze kujirudi.
Ningekuwa mshauri wa JPM, ningemshawishi ahamasishe wananchi katika ku CRITIC anachokifanya ili kukiboresha na si kupenda kusifiwa. Kwa kufanya hivyo ataweza kuwa rais bora kabisa duniani.
Kusifiwa kila kona hupofusha na kuua ubunifu hivyo kubakia kufanya kazi kwa mazoea. Tukumbuke maneno haya “LAITI VIONGOZI TUKIPENDA KUSHANGILIWA HAKIKA HATUTAFIKIA MAENDELEO ENDELEVU” Yosep Stalling, Moscow. Na pia baba wa Taifa alisema “TUNATAKA VIJANA IMARA WENYE KUHOJI” JKNyerere, Dar
Mh. Rais JPM, ukitaka kupiga hatua tena kwa haraka; acha wananchi wahoji (critic) maamuzi yako. Ukitaka kuwa irrelevant basi penda kusifiwa-sifiwa. Jenga Tanzania, vaa ngozi ngumu na ruhusu watu wakukosoe tena hadharani...itakuimarisha sana!
Biashara ya kuhamisha watu eti wanakuunga mkono inakupotezea muda tu kwani haichangii lolote katika ujenzi wa uchumi.
No comments:
Post a Comment