makada wajitokeza kumrithi Kinana. - KULUNZI FIKRA

Friday, 15 December 2017

makada wajitokeza kumrithi Kinana.

 
 Vikao vya sekretariate na Kamati Kuu na kisha NEC vikiwa vinaendelea baadhi ya wajumbe wametajwa katika nafasi ya kumrithi Katibu Mkuu wa sasa Ndugu. Kinana ambaye inasemekana kaomba kupumnzika katika nafasi hiyo.

Wanaotajwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Ndugu Martin Shigela, ambaye pia alishawahi kuhudumu kama Katibu Mkuu wa Vijana Taifa

Wa pili ni Ndugu Pereira ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Idara ya Organization. Pereira anapigiwa upatu kutokana na namna alivyofanikiwa kuendesha uchaguzi wote nchi, na pia kutoka kwake upande wa Zanzibar inasemekana inaweza kumuongezea sifa zaidi.

Wa tatu, ni Prof. Mkumbo ambaye ni Katibu Mkuu wa wizara ya maji kwa sasa. Prof. Mkumbo ni mwanafalsafa nguli na muubiri mzuri wa siasa za ujamaa, hivyo inasemekana anaweza kuendana na Rais Magufuli

Na wa nne anayepigiwa upatu ni Dr. Bashiru Ally. Huyu ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anafahamika kama nguli wa itikadi za kijamaa, mzuri wa kujenga hoja na muumini mkubwa wa Mwalimu Nyerere...

No comments:

Post a Comment

Popular