Familia ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu anayeendelea na matibabu jijini Nairobi imesema tayari imekamilisha kuandika maelezo kujibu barua ya katibu wa Bunge iliyowataka kuainisha haki za ndugu yao wanazozidai kupewa na Bunge kama mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba tayari wameshatuma majibu hayo.
Akizungumza na wanahabari jijini Arusha msemaji wa familia hiyo wakili Alute Mughwai anasema barua hiyo ya Katibu wa Bunge aliipokea Desemba nne mwaka huu.
Bwana Mughwai anasema wamejibu barua hiyo kwa kuzingatia haki za matibabu anazopaswa kupatiwa mbunge wakinukuu kifungu namba ishirini na nne cha sheria ya utawala wa Bunge namba kumi na nne ya mwaka 2008.
Ikiwa ni siku ya mia moja tangu mbunge Tundu Lissu aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi mjini Dodoma familia hiyo imetoa shukrani kwa viongozi na wananchi wote wanaoendelea kumjulia hali wakielekeza shukrani kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi wakieleza kuwa hali ya afya ya Mheshimiwa Lissu imeendelea kuimarika akiendelea na mazoezi wakati familia ikiwa inaendelea kushauriana muda muafaka wa kumsafirisha kwenda nje kwa ajili ya kuimarisha afya yake zaidi.

No comments:
Post a Comment