Zitto kabwe awapigia magoti Watanzania. - KULUNZI FIKRA

Thursday 2 November 2017

Zitto kabwe awapigia magoti Watanzania.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe Zitto Kabwe amewapigia magoti Watanzania na kuwaomba waweze kukichangia chama chake ili waweze kufika katika mikoa 18 kwa lengo la kuzungumzia masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na hali ngumu ya maisha.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kuwa katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika Kata 43 zilizopo kwenye mikoa 18 chama chake cha ACT Wazalendo kimeweka wagombea katika Kata 28 na kwamba kupitia uchaguzi huo ndipo watakapopata nafasi ya kuwaamsha Watanzania kupitia kampeni kukataa uminywaji wa haki za binadamu na kutaka mabadiliko ya Sera za kiuchumi.

"Ndugu Watanzania, Hivi sasa nchi yetu ipo kwenye chaguzi za udiwani kwenye Kata 43 zilizopo kwenye mikoa 18 nchi nzima. Chama chetu cha ACT Wazalendo kimeweka wagombea kwenye kata 28 maeneo mbali mbali nchini. Sisi kama Chama tumeamua kufanya kampeni hizi Kwa kuzungumzia masuala makubwa mawili - ukiukwaji mkubwa wa haki za wananchi na hali ngumu ya maisha ya wananchi.

Lengo kubwa ni kuwaamsha Watanzania kukataa ubinywaji wa haki za binaadamu na kutaka mabadiliko ya sera za uchumi ili kuongeza ajira na kuondoa umasikini. Tutatumia mifano halisi Kwenye kata husika na kutoa sera mbadala Kwa misingi ya Azimio la Tabora' aliandika  Mhe Zitto Kabwe.

Mbali na hilo Zitto Kabwe aliwaomba Watanzania waweze kuchangia kampeni zao
"Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wenye uchungu na Nchi yetu kuchangia kampeni zetu. Tunataka kufika kila ya nchi yetu na wewe ndio utatuwezesha kufika. Chochote ulicho nacho tunaomba utuchangie kwa kutumia namba hizi hapa" alisisitiza Mhe Zitto Kabwe

No comments:

Post a Comment

Popular