Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, leo aliripoti kituo cha Polisi Chang'ombe kama alivyotakiwa baada kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana Oktoba 31, 2017. Baada ya kuripoti Polisi wamemueleza kuwa anapaswa kuripoti tena kituoni hapo Ijumaa ijayo, Novemba 17, 2017.
Kadhia hii inahusisha baadhi ya maneno katika hotuba yake ya Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke. Maneno hayo ni yafuatayo:
1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Ndugu Zitto aliongozana na timu ya mawakili wa chama pamoja na mke wake kituoni Chang'ombe.
Kwa sasa Kiongozi wa Chama anaelekea Kituo cha Polisi Kamata, ambapo Mwenyekiti wa Chama, ndugu Yeremiah Maganja, pamoja na Katibu Mkuu, ndugu Dorothy Semu, wameitikia wito wa Kamishna wa Makosa ya Jinai (DCI) wa Jeshi la Polisi kituoni hapo.
Ado Shaibu - Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi
ACT Wazalendo
Novemba 6, 2017

No comments:
Post a Comment