Msemaji wa serikali: Kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli, Ni mtendaji sio wanasiasa. - KULUNZI FIKRA

Monday, 6 November 2017

Msemaji wa serikali: Kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli, Ni mtendaji sio wanasiasa.

Msemaji wa serikali, Dkt. Abbas amesema mapato ya serikali yameongezeka na isingekuwa na maana kama mapato ya serikali yanaongezeka alafu yanavuja, amedai kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli kwani sio mwanasiasa bali ni mtendaji na anachokisema ndio anachokifanya(Ana ukweli mchungu kuliko ahadi tamu).

Dkt. Abbas ameyasema hayo akiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 ambapo pia ameongelea mapato akitolea mfano mizigo bandarini akisema imeshuka kidogo lakini mapato yameongezeka kutoka bilioni 703 ya zamani mpaka 780 mwaka huu sababu ikiwa mapato kuvuja siku za nyuma.

Kuhusu ndege kushikiliwa, amesema kisheria ndege haijakabidhiwa kwa watanzania na kuhoji wakiishikilia watashikilia ndege ya nani? Amekiri mgogoro huo ulikuwepo lakini wanasheria wameingilia kati na ikifika watawataarifa watanzania kwani ipo katika hatua za mwisho.

Kuhusu watumishi wa umma, amesema mikataba inakuja ambayo itakuwa na malengo na itawafanya watu wakumbuke majukumu yao wakijua wasipoyatimiza kuna hatua zitachukuliwa.

Kuhusu serikali itawaachaje kazi zikiboreshwa! Amesema katika serikali ya awamu ya tano waligundua kuna matatizo makubwa kwenye utumishi, amesema serikali inawajali sana na kuanzia mwezi huu, neema itaanza kuonekana.

Amesema uhakiki wa madeni umefanyika na nusu ya madeni yaliyopolekwa serikali yameonekana hayastahiki kulipwa, amewataka wazabuni wote wanaoidai serikali wawasilishe uthibitisho na madeni hayo yatalipwa. Amesema utaratibu wa sasa, sio kupeleka madeni jumla(Lumpsum) hazina bali taasisi au wizara ikiwasilisha madeni iseme pia nani anawadai na kwa ajili ya nini.

Kuhusu deni la taifa, amesema kwa kawaida mtu anakopa kwa sababu ana uwezo wa kulipa hivyo tunakopesheka, amesema nchi zote duniani zina madeni na mtu anakopa kwa sababu kitu anachotaka kufanya kwa leo, fedha hana ila atazipata.

Amesema kukopa ni kawaida sana na serikali ni tajiri na watu wasibabaike kwani tupo ndani ya kiwango tunachoruhusiwa kukopa.

Kuhusu nishati, amesema ni kweli kuna changamoto lakini miaka mitatu ijayo suala la power bank linakwenda kwisha.

Suala la mikopo, amesema leo vyuo vinafunguliwa na serikali imeshatoa zaidi ya bilioni 400 ikiwemo ada na malazi kwa wanafunzi na robo ya kwanza imeshatoa bilioni 139 na zimeshaenda vyuoni hivyo vyuo vitazisambaza kwa wanafunzi wakifika.

Amesema mshtuko upo kwa baadhi ya watu ambao pesa kwao imepotea lakini changamoto ya mshtuko ipo kwa nchi zote ambazo zilitaka kupiga hatua, amesisitiza pesa wanazopata serikali hawatumii wao bali zinarudishwa kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Popular