Waathirika wa Bomoabomoa inayoendelea katika maeneo ya Kimara hadi Kiluvya, wamemuomba Rais John Magufuli awangalie kwa “jicho la huruma”.
Waathirika hao walitoa kauli hiyo baada ya Rais kutaka zaidi ya nyumba 3,000 jijini Mwanza zisibomolewe kutokana na ushiriki wao katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Wakati ubomoaji nyumba eneo la Kiluvya hadi Kimara unafanywa kupisha upanuzi wa barabara, ubomoaji uliozuiwa Mwanza ulilenga kuondoa wakazi maeneo ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
“Rais ndiye msimamizi mkuu na mwenye mamlaka juu ya ardhi yote nchini kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi namba 4/1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5/1999 na Sheria ya Mipango Miji. Hawa ndiyo wananchi walionipa kura. Naagiza zoezi hilo lisitishwe hadi nitakapotoa maagizo mengine,” alisema Rais akiwa Mwanza.
Kutokana na agizo hilo, wananchi wa maeneo ya Kimara hadi Kiluvya ambao nyumba zao zimebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), wamemuomba Rais awakumbuke.
Mkazi wa Kimara, Juma Ramadhan ambaye nyumba yake ilibomolewa, alisema hata wao walimpigia kura Rais Magufuli hivyo wanamuomba awakumbuke hata kwa fidia.
Hata hivyo, mkazi mwingine wa Kimara, Joseph Lyimo alisema hana shida na kauli ya Rais kwa sababu kesi ya wakazi wa Mwanza haifanani na ya wakazi wa Dar es Salaam.
Alisema wakati Mwanza wananchi wamejenga katika maeneo ya vyombo hivyo vya Serikali, hatua iliyochukuliwa kwa wenzao wa Dar es Salaam ni kwa ajili ya maendeleo na kuondoa msongamano barabarani hivyo anaona ni jambo jema.
Pamoja na hayo, diwani wa Kiluvya, Aidan Kitare alisema baadhi ya waliobomolewa Kimara hadi Kiluvya walikuwa na kesi mahakamani lakini viongozi wa mkoa na wilaya walikaa kimya na kwamba hiyo inaleta picha mbaya.
Mbunge wa Kibamba, Jonh Mnyika alisema kauli ya Rais inamaanisha anawajali zaidi waliompa kura peke yake,” alisema.
“Kama Rais ameona bomoaboamoa ina madhara kwa wakazi wa Mwanza, anachukua hatua gani kuwafidia waliobomolewa Kimara hadi Kiluvya?” alihoji.
“Kama ambavyo walisema hawa wanabomolewa kwa sababu wamejenga maeneo ambayo hayaruhusiwi hata hao wa Mwanza wamejenga maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria,” alisema.
Alisema kwa kuwa Rais amesema anawajali wananchi wake, basi awalipe fidia wananchi wa Kiluvya na Kimara.

No comments:
Post a Comment