Tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania (LHRC), imetamka kuwa ubomoaji wa nyumba za makazi na majengo ya biashara ili kupisha hifadhi ya reli haukuzingatia haki za binadamu na zoezi hilo lilikiuka sheria za kitaifa na kikanda ambazo nchi imeridhia.
Tamko hilo limetolewa baada ya wakazi wa Kata ya Buguruni kwa Mnyamani kubomolewa nyumba zao kwa madai kuwa wapo ndani ya hifadhi ya reli na kuongeza ushahidi uliotolewa kwa upande wa wananchi umedhihirisha matumizi makubwa ya nguvu kutoka jeshi la polisi wakati zoezi hilo likitekelezwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (LHRC), Bahame Nyanduga akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mwandamizi wa tume hiyo, Dastan Nkanabo.
Tume imetoa siku 90 kwa Kampuni ya Rasilimali za Reli (RAHCO) kuwalipa fidia wananchi wa Mnyamani- Buguruni ambao nyumba zao zilibomolewa kimakosa bila kufuata sheria za nchi.

No comments:
Post a Comment