Spika wa Bunge ameiandikia barua tume ya uchaguzi (NEC) kuwa jimbo la Singida Kaskazini liko wazi. - KULUNZI FIKRA

Friday, 3 November 2017

Spika wa Bunge ameiandikia barua tume ya uchaguzi (NEC) kuwa jimbo la Singida Kaskazini liko wazi.

 Spika wa Bunge, Job Ndugai ametangaza kuwa jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa likishilikiwa na Lazaro Nyalandu liko wazi baada ya mbunge huyo kufutwa uanachama na CCM.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Ndugai amemuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi.

Barua hiyo imeandikwa na Spika kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi 2015 kinachoeleza kwamba, pale ambapo mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yeyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha ubunge kiko wazi.

“Kufuatia barua hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi hiyo iliyo wazi,” imeeleza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular