KAMPENI za uchaguzi wa marudio katika kata 43 zinaendelea kwenye mikoa tisa hapa nchini, ambapo wagombea wanaendelea kumwaga sera za vyama vyao huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mara nyingi kampeni za uchaguzi huwa hazikosi vituko mbalimbali vikiwamo vya kupigana vijembe majukwaani na vingine vingi, ambavyo wakati mwingine huchukuliwa kama jambo la kawaida kwenye siasa.
Hata hivyo, wakereketwa na wafurukutwa wa vyama vya kisiasa vinavyoshiriki kwenye chaguzi mbalimbali wakati mwingine hufika mbali zaidi kiasi cha kuzomeana na hata kutishiana kuumizana inapotokea wanakutana wakiwa wamevalia sare za vyama vyao wakielea kwenye kampeni.
Wanasahau kwamba katika mfumo wa siasa za vyama vingi, kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa na hivyo kuvaa sare ya chama chake ni kama jambo la kawaida.
Kimsingi ni vyema zaidi katika medani ya kisiasa kwa upande mwingine mtu akafuata au akaunga mkono chama cha siasa kwa sababu ya sera zake na sio kwa kufuata haiba ya watu ndani ya chama husika.
Sasa kinyume chake, inatokea kuwa baadhi ya wakereketwa na wafurukutwa wa vyama vya siasa wamekuwa wakidhani kwamba mtu ambaye amevaa sare za chama wasichokipenda wanamuona kama adui yao.
Na ndiyo maana mtindo wa kuzomeana kwa sababu tu mtu kavaa sare za chama pinzani wakati akielekea kwenye kampeni, umemkera Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba.
Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, amekemea hali hiyo isiyojenga na kusema kuwa Tanzania inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, unaoruhusiwa na Katiba ya nchi, hivyo kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa anachokitaka.
Kada huyo wa CCM alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Saranga, Haroun Mdoe kupitia chama hicho kwenye ufunguzi wa kampeni uliofanyika mwishoni mwa wiki, Kimara jijini Dar es Salaam.
“Ninasisitiza na kuwaomba mchagueni Mdoe kwa sababu ilani inayotekelezwa kwa sasa ni ya CCM hadi mwaka 2020, hivyo wagombea wengine hawatakuwa na mchango wowote katika maendeleo ya kata hii ya Saranga,” akasema.
Akabainisha kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kila chama kitakuwa na ilani yake na kitakuwa kinatafuta kushika dola na kwamba kwa sasa ilani inayotekelezwa kwa muhula huu ni ya CCM.
SIASA ZA KISTAARABU
Mbali na kumuombea kura mgombea wa chama chake, Nchemba aliwataka wafuasi wa vyama vya siasa na viongozi wao kufanya siasa za kistaarabu kwa kutambua kuwa nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, na kila mtu ana haki ya kujiunga na chama cha siasa anachokitaka.
“Mfumo wa vyama vingi upo kwa zaidi ya miaka 20, inashangaza kuona baadhi ya wafuasi wa vyama wakipishana na wenzao wakati wakielekea katika kampeni na kuanza kuzomeana kiasi cha kulazimu polisi iingilie kati,” akasema na kuongeza:
“Tusibaguane kwa sababu ya sare za vyama, watu wavae sare za vyama vyao waende katika kampeni bila kubughudhiwa na mtu kwani sio kosa kuvaa sare ya chama chako.”
Vilevile kada huyo wa CCM akawataka watambue umuhimu wa kuheshimiana hata kama wakipishina njiani wasalimiane wakati kila mmoja akielekea katika kampeni zake.
“Ni lazima ieleweke kuwa madiwani au wabunge wakishachaguliwa huenda kukutana pamoja kwenye vikao vyao ambako hakuna jengo la wabunge wa upinzani au wa CCM, we ni bungeni au katika baraza la madiwani,” akasema.
Akafafanua kuwa ni kosa mtu kuvaa sare za chama siku ya uchaguzi, lakini vinginevyo yuko huru na hakuna mwenye haki ya kumzomea.
MGOMBEA
Kwa upande wake mgombea udiwani wa chama hicho katika kata hiyo aliahidi kufanya kampeni za kistaarabu, ili hatimaye aibuke na ushindi kwa vile anaamini kwamba vurugu sio sehemu ya ustaarabu wa CCM
“Saranga imekosa maendeleo kwa muda mrefu hivyo ninawaomba wananchi wote wa kata hii mniunge mkono ili niwe mwakilishi wenu na tushirikiane kujiletea maendeleo kwa kukarabati barabara, kuongeza zahanati na miundombinu mingine ya muhimu,” akasema Mdoe.
Mdoe akabainisha kuwa Kata ya Saranga inahitaji kupata kiongozi makini mwenye malengo na mipango ya maendeleo kama yeye (Mdoe) na kwamba umoja ni ushindi, hivyo wakazi wote waungane kuhakikisha anapata ushindi.
“Wana CCM ni watu wastaarabu na nina uhakika kwa ustaarabu wetu na malengo tuliojiwekea kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chetu, wana Saranga watanipa kura niwe diwani wao,” akasema.
Akatoa wito kwa wananchi kuachana na mihemko ya kisiasa kwa kuchagua mgombea mwenye maono na malengo kwa ajili ya maendeleo ya kata yao, ambaye ni yeye (Mdoe).
Kata ya Saranga iko katika jimbo la Kibamba lenye kata 14, huku CCM ikiwa inaongoza kata mbili tu za Mabibo na Mburahati wakati Chadema ina kata 11 za Manzese, Ubungo, Kimara, Mbezi, Kibamba na Goba.
Kata zingine chini ya Chadema ni Kwembe, Msigani, Makuburi, Makurumla na Sinza.
Katika mazingira hayo kila chama kinataka kujinyakulia kata hiyo huku CCM ikitamani kuwa na kata tatu wakati Chadema ambayo inaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo nayo ikitaka kuongeza kata ya 12.

No comments:
Post a Comment