Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru azuia posho kwa madiwani wote wa chadema - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 1 November 2017

Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru azuia posho kwa madiwani wote wa chadema

 MKURUGENZI wa halmashauri ya Meru,Christopher Japhet Kazeri, amezuia madiwani wa Chadema wasilipwe posho,na kuruhusu diwani wa CCM,alipwe baada ya baraza la madiwani kujigeuza kama kamati kwa lengo la kumjadili mkurugenzi huyo kwa tuhuma za ufisadi wa mali za halimashauri hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani wa Halimashauri hiyo lililofanyika katika ofisi za halimashauri hiyo zilizopo Usariver,Wilayani Arumeru,mkoani hapa.

Baada ya madiwani hao kujigeuza kama kamati Mkurugenzi huyo aliamua kususia kikao hicho na kutoka nje pamoja na wakuu wote wa idara na vitengo wa halimashauri hiyo na ndipo alipoelekea katika ofisi za malipo za halimashauri hiyo na kumwuru mhasibu wa halmashauri hiyo kutowalipa madiwani wote wa Chadema.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo,Willy Njau,alisema kuwa kwa muda mrefu sasa mkurugenzi huyo amekuwa akidharau na kulipuuza baraza hilo pamoja na madiwani wake katika maamuzi yote yanayofikiwa katika baraza hilo.

Alizitaja tuhuma za mkurugenzi huyo kuwa ni kuamua kununua gari jipya la mkurugenzi wa halimashauri kwa gharama ya shilingi milioni 140 kinyume na makubaliano ya baraza hilo ya kukarabati gari lililopo kwa gharama ya shilingi milioni 25 na kutumia milioni 55 kununua pikipiki26 kwa ajili ya watendaji wa Kata kinyume na maazimio ya baraza hilo yaliyolenga watendaji wakopeshe pikipiki kwa dhamana ya halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular