Shirika la Ndege la Etihad Airways limemteua Ailende 'Allen' Okoromu kama Meneja Mkaazi ambaye anasimamia Shughuli zote za Shirika hilo nchini Tanzania.
Akiripoti kwa John Friel, Meneja Mkuu wa Shirika la Etihad Airways, anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki na kusini, Bw. Okoromu ataongoza Shirika la Etihad hapa Tanzania likiwa na mikakati mbali mbali ya kujitangaza kibiashara nchini Tanzania, pia kuwajibika kwa kuimarisha zaidi ushirikiano na washirika wa biashara ya usafiri wa anga pamoja na wateja wakubwa wa Shirika hilo.
Okoromu anaanza jukumu hilo jipya jijini Dar es Salaam akitokea kwenye nafasi yake ya awali kama Meneja wa Mauzo wa Shirika la ndege la Etihad nchini Nigeria, ambako alikuwa na jukumu la kuendeleza shughuli za kibiashara za ndege hiyo katika bara la Afrika Kusini mwa Sahara na kanda ya Bahari ya Hindi.
Kabla ya kujiunga na Etihad Airways mwaka 2012, alifanya kazi za mauzo katika vitengo mbalimbali vya juu akiwa katika mashirika ya Aviareps Nigeria Limited na Virgin Nigeria Airways ambako alijenga uelewa wa kina wa masoko biashara na burudani kwa Afrika ya Kati.
John Friel alisema: "Tumejikita kuhakikisha soko letu muhimu sana la Tanzania linakua na ninafurahi kuwa Ailende atakuwa akiongoza timu yetu katika kukuza biashara yetu huko.
Uzoefu wake mkubwa wa biashara na rekodi za mafanikio katika sekta ya anga itakuwa ya thamani sana katika kukuza ufahamu wa Shirika la anga la Etihad, na kumfanya awe mfanyakazi bora wa nafasi hii muhimu mpya nchini Tanzania, ambapo kuna soko lenye nguvu litakalotupa uwezo mkubwa wa kukua zaidi.
Akizungumzia uteuzi wake, Ailende alisema: "Ninafurahi kuchukua nafasi hii mpya nchini Tanzania, ambapo kuna soko lenye nguvu lenye uwezo mkubwa wa kutufanya Etihad kukua zaidi.
"Ninatarajia kufanya kazi na timu hapa kutafuta njia mpya za kupanua ushirika wetu wa kimkakati na ushirikiano wa kibiashara, kuimarisha uhusiano wetu wa kuwapa wateja wetu huduma bora zaidi kwa furaha, na ukarimu.
Shirika la ndege la Etihad lilianza shughuli zake nchini Tanzania Desemba 2015, wakitoa huduma ya kila siku inayoendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 zenye viti 16 katika daraja la pili/biashara na viti 120 kwa ndege darja la Uchumi. Dar es Salaam ni njia ya tatu ya ndege kwa nchi za Afrika Mashariki, ikijumuisha Nairobi nchini Kenya, na Entebbe, Uganda.

No comments:
Post a Comment