Mbunge Leonidas Gama amezikwa kijijini kwao. - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 28 November 2017

Mbunge Leonidas Gama amezikwa kijijini kwao.

 
 Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama anazikwa Jana kijijini kwao Likuyu Fusi wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Ibada ya mazishi imefanyika Jana Jumatatu Novemba 27,2017 nyumbani kwao kijijini Likuyu Fusi umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Gama alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi Novemba 23,2017 katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho alikopelekwa baada ya hali yake kubadilika akiwa nyumbani kwake.

Taarifa ya Bunge iliyotolewa baada ya kifo cha Gama ilisema mbunge huyo alirejea nchini Novemba 11,2017 akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Novemba 21,2017 Gama akitokea Dar es Salaam kurejea Songea alipitia Dodoma ili kushiriki mapokezi ya ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa iliyoanza Novemba 23,2017.

Taarifa ya Bunge ilisema Novemba 22,2017 aliugua ghafla na baada ya ofisi ya Bunge kupata taarifa iliandaa ndege maalumu kwa ajili ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, madaktari wa Peramiho walishauri asisafirishwe hadi hali yake itakapotengamaa.

No comments:

Post a Comment

Popular