Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA, Lawrence Masha ameomba kupokelewa katika chama chake cha zamani cha CCM alichokihama wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Lawrence Masha amejiunga leo jumanne na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vikao vya Chama hicho vinavyoendelea Ikulu jijini Dar es salaam na kusema kuwa ”Nimekuja hapa kuwaombeni mnipokee mwana mpotevu nimerudi, Niko imara na nitakuwa mwaminifu kwa CCM.”
Naye, Wakili Msomi aliyewahi kuwa mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Albert Msando amejiunga na Chama Cha Mapinduzi katika vikao hicho vinavyoendelea Ikulu.
Katika hali nyingine ya kushangaza ni kwa Kiongozi mkubwa wa Baraza la vijana wa CHADEMA Taifa, Patrobas Katambi naye ametangaza kuachana na CHADEMA na kujiunga rasmi CCM.

No comments:
Post a Comment