Kilimanjaro: Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Noah kugongana na Lori. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 11 November 2017

Kilimanjaro: Watu wanne wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Noah kugongana na Lori.

 
 Watu wanne wamedaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya magari mawili Toyota Noah na Lori la maji kugongana katika maeneo ya Kikafu, Sadala mkoani Kilimanjaro.

Ajali hiyo mbaya inadaiwa kutokea mchana wa leo ambayo imesababishwa na Lori hilo lililokuwa likijaribu kulipita gari la mbele, na kisha kukutana uso kwa uso na gari hilo ndogo iliyokuwa imebeba abiria ikitokea mjini Moshi ikielekea Sanya Juu.

No comments:

Post a Comment

Popular