Kampuni ya udalali ya Yono wameifunga hoteli ya Blue Pearl ya jijini Dar es salaam, Leo alhamisi Novemba 9, kutokana na kudaiwa kodi ya Pango ya sh 5.7 bilioni.
Hoteli hiyo inadaiwa kodi hiyo na kampuni ya ubungo plaza ambayo inamilikiwa kwa ubia na shirika la Bima la Taifa (NIC) shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) na mfumo wa pesheni PSPF.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scholastika Kevela, amesema walipewa kazi ya kuifungia hoteli hiyo na hatua nyingine za kisheria zitafuata endapo watashindwa kulipa deni hilo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya ubungo plaza, Harun Mgade, amesema mpangaji huyo alikuwa na mikataba wa miaka 15 toka mwaka 2006 lakini tangu mwaka 2014 hajalipa kodi ya pango.
Katika kuonyesha hawatanii, kampuni ya ya Yono walifuta maandishi ya mabango ya hoteli hiyo, huku baadhi ya wageni waliokuwa wamelala hoteli hapo walikutwa na taharuki wasijue nini cha kufanya wakati wengine wakijiandaa kuondoka hotelini hapo.

No comments:
Post a Comment