Katika halo isiyo ya kawaida jeshi la polisi leo limefika na kuzingira nyumbani kwa Mhe Edward Lowassa na nakuzuia wafuasi waliokuwa wamefika nyumbani kwake kwaajili ya kumsidikiza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Muda wilaya ya Arumeru.
Kutokana na kitendo hicho baadhi ya wafuasi na viongozi walifika nyumbani kwa Mhe Edward Lowassa walianza kulalamika na kusema kitendo kama hiki akifai kwa jeshi la polisi linakibeba chama cha mapinduzi (CCM).
"Katika kuonyesha kuwa CCM inahofu katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani ,magari zaidi ya 10 ya jeshi la Polisi mkoa wa Arusha yamezunguka nyumba ya Lowassa ambae ni waziri Mkuu mstaafu na kuzuia msafara wa Magari na pikipiki kuelekea kata ya musa wilaya ya Arumeru kumnadi mgombea udiwani," alisema mmoja wa viongozi.
Tukio hilo limejiri Leo jumatatu kuanzia majira ya saa 9 alasiri ambapo Polisi wenye silaha na mabomu walitanda nyumbani kwa Lowassa Monduli, kwa lengo la kumzuia asiende kwenye Mkutano wa kampeni kumnadi mgombea udiwani.
Aidha wafuasi wa chadema waliomfuata kumpokea wakiwemo viongozi walizuiwa na Polisi huku Katibu mwenezi wa jimbo la Arumeru mashariki John Seneu akitiwa mbaroni na Polisi.
"Hatua hii ni hofu kwa chama cha mapinduzi ( CCM) zinazopelekea kutumia vyombo vya dola vibaya kwaajili ya kupunguza nguvu za wapinzani badala ya kuacha tushindane kwa hoja na sio kutumia nguvu za vyombo vya dola kama hivi" alisema mwanachama wa chadema.

No comments:
Post a Comment