Dkt Louis Shika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kushindwa zabuni ya kununua nyumba tatu za kifahari za kwa takribani Tsh 3 bilioni lakini akashindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo, amedai ameanza mchakato wa kurejesha fedha zake zilizo nje ya nchi.
Dkt Shika amedai jana jumamosi Novemba 18, 2017 kuwa amelipa dola 100 za kimarekani (sawa na Tsh 220,000 za kitanzania ) kwaajili ya bima ili aweze kutumiwa fedha zake nchini.
Dkt Shika alifanikiwa kuzungumza na waandishi wa habari hapo jana walipokuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa uchukuzi na mawasiliano, Atashasta Nditiye aliyeenda kutembelea shirika la posta kuzungumza na wafanyakazi.
Waandishi wa habari walimkutu Dkt Shika akiwa katika shirika hilo akifanya mchakato wa kutuma malipo ya bima.
Dkt Shika ambaye alishikiliwa na polisi kwaajili ya mahojiano akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabiashara maarufu jijini Dar es salaam, Said Lugumi, alisema ametumia shirika la posta kulipia fedha hizo za bima kwa benki moja iliyopo Bangkok Thailand.
"Kama mnavyoona hii karatasi ni ya malipo ya bima" alisema akionyesha fomu ya malipo
"Nimelipa dola 100 za bima ili kukamilisha malipo ya bima ili fedha zangu zije mapema na niweze kulipia zile nyumba. Hili la bima lilikuwa ni muhimu sana" alisema Dkt Shika.
Hata hivyo, moja ya nyumba hizo tatu ilishauzwa kwa mshindi wa pili kwenye mnada huo, wakati kampuni ya udalali ya Yono imesema itaendesha tena mnada mwingine kuuza nyumba zilizosalia.
'Bilionea' huyo akuelezea fedha alizolipia ni kwaajili ya kuongoza kiasi gani nchini cha fedha.
Dkt Shika amesema bado anaamini kwamba nyumba hizo atazimiliki ili kuwaziba midomo wale wote wanaombeza kwamba hana fedha.

No comments:
Post a Comment