Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vincent Mashinji amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kueleza sababu za kumkamata na kumshikilia kinyume cha sheria mgombea udiwani wa CHADEMA katika Kata ya Mhandu, Godfrey Misana katikati ya kampeni.
Amesema kuwa iwapo jeshi hilo litaendelea kumshikilia mgombea huyo huku likimnyima dhamana na hivyo kushindwa kuendelea na kampeni, chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya njama hizo za kuvuruga uchaguzi huo.
Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza baada ya jeshi hilo kumkamata na kumshikilia mgombea udiwani wa CHADEMA katika kata hiyo,Godfrey Misana kwa mara ya pili leo mchana na kumnyima dhamana bila kueleza sababu yoyote ya kufanya hivyo.
Jeshi hilo lilimkamata Godfrey Misana jana jioni baada ya mkutano wa kampeni na kumshikilia rumande hadi lilipomwachia leo kabla ya kumkamata tena baadae mchana.
Akitoa kauli hiyo mbele ya na viongozi na wanachama wa Kata ya Mhandu aliokutana nao katika kikao cha ndani kuzungumzia hali ya kampeni za uchaguzi huo, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji amewataka kuwa tayari kuzikabili changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na hujuma za chama tawala kupitia vyombo vya dola.
Dkt. Mashinji aliwataka wakazi wa Kata ya Mhandu kutokata tamaa kutokana na hila kama hizo za polisi kumkamata na kumshikilia kinyume cha sheria mgombea wa CHADEMA hivyo kumzuia kufanya kampeni.
Akisisitiza kuwa CHADEMA kimejiandaa kufanya kampeni za ushindani na kushinda uchaguzi huo wa marudio, Dkt. Mashinji amewaagiza viongozi wa chama na wanachama kuwafikia wapiga kura kwa kila njia kumnadi mgombea ili kufanikisha ushindi huo.

No comments:
Post a Comment