Anayetumiwa kuwa watu wawili katika nyumba ya wageni Tanga a - KULUNZI FIKRA

Friday 3 November 2017

Anayetumiwa kuwa watu wawili katika nyumba ya wageni Tanga a

 Mkazi wa Kijiji cha Bulwa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza, Ismail Yahaya (41) aliyekamatwa Tunduma wiki iliyopita akifanya jaribio la kutaka kutoroka nchini, hatimaye amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Tanga na kusomewa mashtaka mawili ya mauaji.

Ismail ambaye ni mganga wa jadi alifikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Tanga, Crisencia Kisongo akituhumiwa kuwaua Ibrahim Ali na Benedictor John katika nyumba ya kulala wageni.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Rebeca Msalangi mbele ya hakimu huyo kuwa mshtakiwa huyo alifanya mauaji hayo Septemba 25 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo Bomai Inn iliyopo barabara ya 20 jijini hapa.

Wakili huyo wa Serikali aliendelea kudai shtaka la kwanza linalomkabili mshtakiwa huyo ni kuwa Septemba 25 alimuua Ibrahim Ali na kisha kumfunga kamba. Shitaka la pili kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo ni kwamba Septemba 25 mwaka huu mshtakiwa huyo alimuua Benedictor John na kasha kumfunga kamba.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu Cresencia alisema kutokana na kesi hiyo kuwa ya mauaji, mshtakiwa hakustahili kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria hadi itakapofikishwa ngazi ya mahakama kuu.

"Kwa sababu hiyo huwezi pia kupewa dhamana kwa hiyo utakwenda Rumande," alisema hakimu huyo wakati akiahirisha kesi hiyo hiyo hadi itakapotajwa tena Novemba 14 mwaka huu

No comments:

Post a Comment

Popular