Chama cha ACT Wazalendo kimeweka wazi msimamo wake kuhusu suala la kujiunga na UKAWA ambapo kimesema suala hilo ni pana na lazima lizingatie maslahi ya chama.
Akiongea leo kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio, Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho Ado Shaibu, amesema suala la kujiunga au kutojiunga UKAWA litaamuliwa na wanachama na viongozi.
“Ni kweli kila mtu anazungumza yake kuhusu msimamo wa chama chetu lakini ukweli ni kwamba kwa hali ya kisiasa ilivyo nchini kuna mambo yanalazimu vyama vya upinzani vishirikiane, lakini ikija suala la kujiunga UKAWA lazima ujue maslahi ya chama ndani ya umoja huo”, amesema Ado Shaibu.
Ado ameongeza kuwa ikifikia wakati kuna ulazima wa ACT Wazalendo kujiunga na UKAWA basi suala hilo litaamuliwa na viongozi pamoja na wanachama.
Kwa upande mwingine Shaibu amewataka wanachama wa ACT Wazalendo kuendelea kukiunga mkono chama hicho wakati huu ambao sera zake zimejikita zaidi kwenye kuutafuta uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara kwani ndio njia pekee ya kuongea na wananchi moja kwa moja.

No comments:
Post a Comment