Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa jana na kampuni ya Barrick Gold Mining, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.
Akifanya mahojiano maalalumu leo mchana, Mh. Kabwe amesema kwamba alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (ameiita kishika uchumba) kwani hata 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi.
Mh. Zitto amesema kwamba tangu jana alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba "Tumefanikiwa" kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.
"Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo".
Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Friday, 20 October 2017
Home
Unlabelled
Zitto kabwe: Serikali ilikosea kutangaza mapema
Zitto kabwe: Serikali ilikosea kutangaza mapema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment