Dkt Jakaya Kikwete afunguka kuhusiana na kinachokwamisha Bara la Afrika - KULUNZI FIKRA

Friday, 20 October 2017

Dkt Jakaya Kikwete afunguka kuhusiana na kinachokwamisha Bara la Afrika

 Rais Mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema uchangishaji fedha kwa ajili ya miundombinu na kilimo ni lazima uende kwa pamoja kwa sababu masuala hayo ni masuala mtambuka kwa maendeleo ya taifa lolote duniani.

Dk. Kikwete amesema hayo leo wakati akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini New York, nchini Marekani, baada ya kushiriki kikao cha ngazi ya juu cha Wiki ya Afrika ambapo masuala ya tabianchi, miundombinu, kilimo na vijana yamejadiliwa.

Dk. Kikwete amesema uchangishaji usiotosheleza wa fedha katika sekta ya kilimo unakwamisha wakulima kushiriki kilimo cha kisasa kwa kutumia mbegu zisizo na ubora na kusababisha wakulima kukosa mavuno yenye tija.

"Ukiendeleza kilimo unasaidia watu wengi sana na umasikini wa Afrika una sura ya vijijini kwamba masikini wengi waliopo Afrika wapo vijijini na tatizo kubwa la kilimo ni kwamba tunatumia dhana za zamani jembe la mkono linatumika zaidi kuliko mashine na mitambo, asilimia 4 tu ya kilimo chetu tunatumia umwagiliaji na mvua ya Mwenyezi Mungu, tatu kilimo chetu hatutumii mbegu bora tunatumia mbegu za asili ambazo hazizalishi sana", alisema Dk. Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Popular