Wakati juhudi za kuagiza vipuli vya magari yaendayo haraka (UDART) zikifanyika ili yarejee barabarani kutokana na uharibifu uliosababishwa na mvua zilizonyeesha mwishoni mwa wiki hii Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jafo ameagiza
kampuni hiyo kushirikiana na Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) kuyahamisha magari maegesho ya dharura ili kuepusha uharibifu zaidi.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo hii baada ya kutembelea eneo la Jangwani, Jijini Dar es salaam yalipo maegesho ya mabasi hayo ambapo amesema kwamba maegesho hayo yameshapatikana na hivyo kuwataka kufanya hima kwa ajili ya usalama wa mabasi hayo ambayo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Dar es salaam.
Mbali na hayo Waziri Jafo ameitaka UDART, DART pamoja na DAWASA wasafishe mto Msimbazi ili kuruhusu maji ya mvua yapite kirahisi ili kuweza kufanya marekebisho ndani ya maegesho hayo ambapo pia maeneo hayo wapo wananchi wa kawaida.
Pamoja na hayo waziri Jafo amewataka wasimamizi wa mabasi hayo yaendayo haraka waweze kuboresha maeneo yao kwa ubora mzuri ili kuzuia uharibifu unaoweza kufanywa na mvua wakati mwingine
Aidha waziri Jaffo ameweka wazi kwamba idadi ya mabasi yanayokwenda haraka yaliyoharibika kutokana mvua kubwa iliyonyeesha mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam ni zaidi ya 30.
Mabasi hayo ni yale yaliyoegeshwa katika eneo la Jangwani yalupo maegesho ya mabasi hayo jijini Dar es salaam

No comments:
Post a Comment